Friday, December 9, 2011

SHEREHE ZA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA(UHURU DAY)



Mnamo majira ya saa 6.05 usiku tarehe 09 dec 2011,ilisikika milio ya mizinga ikitokea iwanja cha uhuru maeneo ya temeke na pia fataki kutoka viwanja vya mnazi mmoja kuashiria ile siku iliyokuwa ikisubiriwa na watanzania kwa hamu kubwa imewadia,Siku ya kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa taifa la Tanzania.

Asubuhi ya tarehe 9 dec ,imekuwa ya shamra shamra nyingi ambapo kwa wingi wananchi wameweza kufurika katika uwanja huu ,wakubwa kwa wadogo ili kuweza kuwa moja ya mashuhuda wa tukio hili .Wakati huohuo pia wakuu wa nchi mbalimbali ,mabalozi ,wawakilishi toka sekta mbalimbali ndani na nje ya nchi wamehudhuria katika maadhimisho haya.

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania,Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete aliwasili kiwanjani hapa ,na ndipo shughuli nzima ilipoanza,ambapo aliweza kukagua gwaride na baada ya wimbo wa Taifa aliweza kwenda mahala pake na kuketi.

Mpaka wakati huu kuna maonnyesho mbalimbali ya kuvutia ,kama ngoma,nyimbo za kitamaduni ,na kumalizia na wimbo wa miaka 50 ya uhuru wa tanzania kutoka kwa muungano wa vikundi vya injili nchini.

Ndipo baada ya yote hayo saa 7.45 mchana,Mhe.Rais Jakhaya Kikwete alisimama ili kuwezakutoa hotuba yake,na kuanza kwa shukrani kwa mwenyezi mungu na kutoa maelezo ya uhuru wa nchi yetu na kusema bayana kuwa kwa ujumla sherehe za uhuru za mwaka huu zimefana sana katika kipindi chote hiki.

Ndipo salamu za shukrani kwa watanzania kwa ujumla na wahusika waliohusika katika kuratibu sherehe hizo ,na kufanikiwa pamoja na changamoto mbalimbali zilizoweza kuwakuta.Pia aliwashukuru wageni wote walioweza kufika katika maadhimisho haya na kusema kuwa hicho ni kielelezo kizuri cha uhusiano bora uliopo kati ya nchi na wao na pia kuahidi kudumisha uhusiano huo.

Aliweza kutoa shukrani zake za dhati kwa wazee 17 ambao ndio waliofanikisha Uhuru wa Tanganyika ,wakiongozwa na Hayati Mwl.Julias Kambarage Nyerere,ambapo bila wazee hao pengine nchi yetu ingekuwa chini ya utawala wa waingereza mpaka leo hii.

Rais pia alisema kuwa nchi yetu kwa sasa ni yenye uhuru na maamuzi yake binafsi bila kuingiliwa na pande yoyote,nchi pia ina mafanikio makubwa ya japo kuwa kubwa na makibila mengi imeweza kudumisha uhuru na upendo na yote haya ni juu ya sera bora.
Nchi imeweza kupambana na ujinga na umasikini na mafanikio ni makubwa sana ukilinganisha na jinsi tulivyoachwa na wakoloni.Lakini pamoja na mafanikio haya bado kuna makubwa sana yanayopaswa kufanywa ili kuweza kujipatia mafanikio nchi zaidi.Cha msingi ni kufanya kazi kwa bidii na kutokata tamaa.Mheshimiwa alifunga hotuba ya kwa mbiu
"HAKIKA TUMETHUBUTU,HAKIKA TUMEWEZA NA HAKIKA TUNAZIDI KUNASONGA MBELE".