Wednesday, November 30, 2011
Mwanafunzi Tudarco na aliyekuwa mfanyakazi wa TBC ,Jerry Murro ashinda kesi.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemwachia huru kwa mashitaka yote matatu yaliyokuwa yakimkabili aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Jarry Muro na pia mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Tumaini Dar es salaam.
Mshitakiwa huyo ameeachiwa baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi ya mtuhumiwa huyo,alisema Hakimu Frank Moshi.
Muro, na wenzake walikuwa wakikabiliwa na kesi ya kuomba na kutaka kupokea rushwa ya Sh milioni 10 toka kwa aliyekuwa Muhasibu wa Wilaya ya Bagamoyo Michael Wage.
Mashitaka yao yalikuwa ni ya kula njama, kuomba rushwa na kujitambulisha maafisa wa TAKUKURU shitaka linalowakabili Mgasa na kapama.
Baada ya kutoka mahakamani Muro alitangaza kwa waandishi wa habari kuwasamehe wale wote ambao kwa namna moja au nyingine walikuwa na nia ya kuharibu jina na maisha yake na pia aliwasihi waandishi wa habari kushikamana kuendelea kuibua uozo unaoendelea bila woga wa aina yoyote.
Ushahidi dhidi ya washitakiwa toka kwa jamhuri ulikuwa finyu na ambao haukuwa umekamilika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment